Wanufaika wa mrafdi wa FOSENI II/ Uhakika wa Chakila na Uboreshaji Lishe unaotekelezwa na shirika la Uwiano wa Maendeleo Vijijini/IRDO katika vijiji 11 vilivyopo wilya ya Ileje mkoa wa Songwe. wamekabidhiwa kuku na mratibu wa mradi huo Bw. Gaster Kihwello ikiwa ni kwaajili ya kufuga kwa lengo la kujipatia kipato kutokana na kuuza mayai ya kuku baada ya kuzaliana iliwaweze kuendesha maisha yao, Kupitia ufugaji wa kuku wanufaika wanaboresha lishe kwa kula nyama na mayai yatokanayo na ufugaji huo. IRDO inaunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na Udumavu mkoa wa Songwe